Kupitia jukumu hilo Mamlaka imeiongezea Serikali mapato katika mizigo ambayo inasafirishwa kutoka nchini kwenda nje ya nchi lakini pia kufanikiwa kufungua masoko mbalimbali ya bidhaa ambayo nchi yetu ilifungiwa kutokana na kutokidhi mahitaji ya masoko yao na sasa watanzania na makampuni yanauza mazao yetu kwa wingi kwenye masoko hayo.
Amesema ushirikiano kati ya TPHPA na Wizara ya Mambo ya Nje ni muhimu katika kuhakikisha mazao ya Tanzania yanapata masoko ya uhakika nje ya nchi.