Winga wa kimataifa wa Brazil, Vinicius Jr, amekubaliana na klabu ya Real Madrid kuongeza mkataba mpya wa miaka sita utakaomuweka Santiago Bernabeu hadi Juni 30, 2032.
Real Madrid imekomesha uvumi wa muda mrefu kuhusu mustakabali wa Vinicius Jr baada ya kutangaza rasmi kuongeza mkataba wa winga huyo wa kimataifa wa Brazil hadi Juni 30, 2032.