Akizungumzia Kaulimbiu ya Mwaka huu ya 'Tambua Soko, Ongeza Tija, Kutekeleza Dira 2050', Mhe. Mzava amesema utekelezaji wake unapaswa kuanzia kwenye Mbegu na namna wakulima na wafugaji wanavyohudumia mashamba na mifugo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ya 'Tambua soko, ongeza tija kutekeleza Dira ya 2050' inahimiza wakulima na wafugaji kwamba kabla ya kuzalisha ni muhimu kuanzia sokoni ili kutambua mahitaji ya soko kwa lengo la kuzalisha bidhaa zenye ubora kwa kuzingatia ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi.