Dk. Samia amesema bara hilo limekuwa na maono na mipango mbalimbali ya maendeleo kwa muda mrefu, lakini sasa kinachohitajika ni utekelezaji wa miradi yenye matokeo yanayoonekana katika maisha ya wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa viongozi wa nchi za Afrika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya miundombinu, akisisitiza kuwa maendeleo ya Bara hilo hayatapimwa kwa mipango na sera pekee, bali kwa matokeo yanayoonekana katika maisha ya wananchi.