Akiwa kwenye Banda la NSSF, Rais amefurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na NSSF hususan katika kuboresha huduma kwa wanachama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Tamasha la Kizimkazi, ambapo alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba. Pamoja na kutembelea banda la Mfuko, Mhe. Rais alitembelea mabanda mengine ya taasisi na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa. Mhe. Rais amefurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na NSSF hususan katika kuboresha huduma kwa wanachama.