PPRA imeanzisha programu ya simu inayojulikana kama NeST Tenderer, inayopatikana kupitia Play Store na App Store.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeendelea kurahisisha upatikanaji wa fursa za zabuni za Serikali kwa kuanzisha programu ya simu janja ya NeST Tenderer, inayolenga kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kushiriki katika ununuzi wa umma kwa urahisi zaidi.