Rais Samia amezindua pia Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 na kukabidhi Ufunguo wa Mtazamo Mpya, unaoashiria mwanzo mpya wa ushirikiano wenye uwazi na uaminifu kati ya Serikali na Sekta Binafsi.
Miongoni mwa nyenzo zilizozinduliwa ni Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu wa miaka 25, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP IV), Mwongozo wa Kitaifa wa Upimaji wa Matokeo ya Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo pamoja na Mkakati wa Mawasiliano wa Dira 2050.
Katika hafla hiyo, Rais Samia pia alishuhudia utiaji saini wa Tamko la Pamoja kati ya Serikali na Sekta Binafsi kuhusu utekelezaji wa Dira 2050.