Kisima cha Maji Safi na Salama Kijiji cha Makulu
Latest Tanzania water sanitation news · Kisima cha Maji Safi na Salama Kijiji cha Makulu explained · updated Aug 7, 2026 · breaking news · latest updates · explained
TLDR
- DODOMA: Mkurugenzi wa Taasisi ya Igambilo, Gerald Ntyama, amesema taasisi hiyo imeendelea kuboresha maisha ya wananchi wa Kijiji cha Makulu, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kupitia utekelezaji wa miradi ya maji safi.
- Ntyama amesema hayo katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Dodoma, akieleza kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kujenga kisima cha maji safi na salama kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa, wananchi wa.
- Amesema mchango wa taasisi hiyo ya ufadhili umekuwa wa muhimu katika kuhakikisha wananchi wa Makulu wanapata huduma ya maji safi na salama pamoja na fursa za maendeleo endelevu.
- Ameeleza kuwa kabla ya mradi huo, wakazi walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata maji kutoka katika vyanzo visivyo salama, hali iliyochangia kuongezeka kwa magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji machafu.
- Amesema upatikanaji wa maji kutoka kwenye kisima umeleta nafuu kubwa kwa wanawake na watoto waliokuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji, huku ukiwapa nafasi ya kushiriki katika shughuli nyingine za maendeleo.