Nyota wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Jamal Musiala, amethibitisha kuwa amegunduliwa na tatizo la kiafya linaloitwa absence seizures baada ya kuanguka mara mbili ndani ya siku nne kwenye mechi za maandalizi ya msimu.
Musiala amefichua kuwa anapata matibabu kutokana na hali ya absence seizures (vipindi vifupi vya kupoteza ufahamu) baada ya kuanguka uwanjani mara mbili ndani ya siku nne.