Amesema mbali na uchunguzi wa sampuli, GST pia inafanya tafiti za uchenjuaji wa madini kwa lengo la kumsaidia mchimbaji kutumia njia sahihi za uchimbaji na uchenjuaji ili kuongeza kiwango cha madini anachopata na kupunguza upotevu wa madini.
Wachimbaji wengi wamekuwa wakipoteza madini mengi yaliyopo kwenye miamba kutokana na kutofanya tafiti bora za uchenjuaji.