Fursa hizo zinatokana na maboresho yaliyofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ikiwamo upanuzi wa gati uliowezesha meli kubwa kutia nanga kupakia na kushusha mizigo mbalimbali.
Ngezi alisema gati zimeongezwa kutoka tatu hadi nne, huku gati moja likiwa na urefu wa mita 300 na kina cha maji cha mita 13, hali inayowezesha meli kubwa kutia nanga na kupakia au kushusha shehena nyingi zaidi.