Waziri Mkuu amewahimiza vijana nchini kutumia fursa zilizopo katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuwekeza katika uzalishaji wa kisasa unaotumia teknolojia na ubunifu.
Aidha, aliwataka vijana kuendelea kutumia elimu, maarifa na ubunifu kuwekeza katika kilimo na ufugaji wa kisasa ili kujiongezea kipato, kuzalisha ajira na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.