Mhe. Chongolo pia amepongeza uamuzi wa Serikali kujenga uwanja huo nje ya Jiji, akisema katika utekelezaji wake, fursa za uwekezaji zitafunguka zaidi hasa pia kutokana na kuwepo kwa ujenzi wa Kituo kikuu cha Mabasi Jiji la Arusha ambacho nacho kinajengwa kwenye Kata ya Olmot.
Waziri wa Kilimo na Mlezi wa Kiserikali wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daniel Godfrey Chongolo amemshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha Arusha kuwa sehemu ya Mwenyeji wa michuano ya soka kwa timu za Taifa za wanaume AFCON 2027, akisema kibali hicho kimesaidia kusukuma masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara.