Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alisema watu sita walifariki dunia katika ajali hiyo ambapo watano walipoteza maisha papo hapo na mmoja alifariki akiwa anapatiwa matibabu hospitalini.
Katika hatua nyingine, Julai 30, mwaka huu, watu sita walipoteza maisha kutokana na ajali iliyohusisha basi lililogongana na lori wilayani Monduli mkoani Arusha.