Pia alishiriki maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) pamoja na shughuli za Siku ya Ushirika, akisisitiza umuhimu wa utafiti na ubunifu katika kuimarisha uchumi na usalama wa chakula Nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe.Daniel Chongolo (Mb) leo tarehe 02 Agosti 2026,ameongoza mamia ya washiriki katika Marathon ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Katika Viwanja vya Dkt.Samweli Malecela Nane Nane Nzuguni jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo.