Amesema mahitaji ya nyumba katika Jiji la Dodoma ni makubwa, akifichua kuwa wakati ujenzi wa nyumba 150 za awali ulipokuwa ukiendelea, TBA ilipokea zaidi ya maombi 1,000 kutoka kwa watumishi waliokuwa wakihitaji makazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Miliki wa TBA, Said Rajabu Mndeme, aliyemwakilisha Mtendaji Mkuu wa TBA, amesema mradi huo unatekelezwa katika eneo lenye takribani ekari 640, ambapo ujenzi wa nyumba 150 tayari umekamilika.