Mada zilizoorodheshwa
LAW JUSTICE 1 nukuu · 1 makala · 1 vyanzo

Peter Madeleka Charged with Five Counts of Contempt of Court

Habari mpya za law justice Tanzania · maelezo ya Peter Madeleka Charged with Five Counts of Contempt of… · masasisho 2026 · imesasishwa 20 Aug 2026 · habari mpya · masasisho · maelezo

Muhtasari

  • Peter Madeleka, wakili wa kujitegemea, amefikishwa mahakamani kwa mashtaka matano ya kuidharau mahakama katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.
  • Mashtaka hayo yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Hassan Makube, huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Job Mrema na wengine.
  • Shtaka la kwanza linadai kuwa tarehe 27 Julai 2026, Madeleka alichapisha taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kesi aliyokuwa akitetea, akikiuka amri ya mahakama.
  • Shtaka la pili linadai kuwa tarehe 28 Julai 2026, alichapisha tena taarifa kuhusu kesi hiyo, jambo ambalo pia lilikiuka amri ya mahakama.
  • Shtaka la tatu linahusiana na taarifa alizotoa tarehe 7 Agosti 2026, wakati kesi hiyo ilikuwa bado inaendelea katika Mahakama Kuu.

Nukuu za habari mpya na vyanzo: Peter Madeleka Charged with Five Counts of Contempt of…

ippmedia.co.tzSoma zaidi

Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka, amefikishwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka matano ya kuidharau Mahakama. Madeleka amefikishwa mahakamani leo jioni mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Hassan Makube, ambapo Jamhuri imewakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Job Mrema, akisaidiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi Clemence Kato, Moseie Kaima na Veronica Chacha. Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Kato amedai kuwa Julai 27, 2026, eneo la Mawasiliano, Wilaya ya Ubungo, Madeleka akiwa wakili wa utetezi katika Kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 4521/2026, Jamhuri dhidi ya Wendy Ishengoma na wenzake wanne, alitoa na kuchapisha kauli katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo Jambo TV, kuhusu kesi hiyo. Imedaiwa kuwa kitendo hicho kilikiuka na kudharau amri ya Mahakama iliyotolewa Julai 27, 2026, na Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Makosa ya Uhujumu Uchumi. Katika shtaka la pili, Madeleka anadaiwa Julai 28, 2026, katika eneo hilo hilo, kutoa na kuchapisha kauli kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ikiwemo Jambo TV kuhusu kesi hiyo, kitendo ambacho kinadaiwa kilikiuka amri ya Mahakama. Shtaka la tatu linahusiana na Agosti 7, 2026, ambapo Madeleka anadaiwa akiwa Mikocheni, Wilaya ya Kinondoni, kutoa na kuchapisha kauli kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kesi hiyo wakati bado ikiendelea Mahakama Kuu. Katika shtaka la nne, Madeleka anadaiwa Agosti 7, 2026, kutoa kauli kupitia vyombo vya habari ikiwemo Jambo TV kuhusu mwenendo wa kesi hiyo, ambayo upande wa mashtaka unadai ilipotosha mwenendo wa kesi. Katika shtaka hilo, alidaiwa kusema kuwa 'Mawakili wa Serikali walikuwa wanaomba vielelezo vilivyotolewa mahakamani vikahifadhiwe kwenye Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,' huku akijua kuwa kauli hiyo haikuwa ya kweli. Shtaka la tano linahusiana na Agosti 13, 2026, ambapo Madeleka anadaiwa akiwa Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, kutoa na kuchapisha kauli kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Jambo TV kuhusu kesi hiyo, kitendo kinachodaiwa kudharau amri ya Mahakama iliyotolewa Julai 27, 2026.

Uliza chochote kuhusu mada hii — mfululizo, athari, wahusika, au uhusiano na Tanzania.