Akifunga maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, Dkt. Salekwa amesema kuwa matumizi sahihi ya pembejeo, mbinu bora za kilimo na teknolojia za kisasa ni muhimu katika kuongeza uzalishaji na kuboresha maisha ya wakulima.
Mhe. Kheri amesema matumizi ya teknolojia za kisasa katika kilimo yatasaidia kuongeza tija ya uzalishaji, kupunguza changamoto zinazowakabili wakulima na kuongeza ubora pamoja na thamani ya mazao yanayozalishwa mkoani Iringa.