Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dkt. Linda Salekwa, Agosti 10, 2026 amefunga Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika katika Kata ya Mlenge, Tarafa ya Pawaga, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, akiwataka wakulima kutumia pembejeo bora pamoja na teknolojia za kisasa za kilimo ili kuongeza tija na kupunguza uzalishaji duni.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, ametoa wito kwa Mkoa wa Iringa kuhakikisha ubunifu na teknolojia mbalimbali zinazooneshwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane zinamfikia Mwananchi mmoja mmoja, ili kuongeza tija na kuchochea uzalishaji katika sekta ya kilimo.