Kuna malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi kuhusiana na suala la utoaji wa fedha ambazo zinatolewa na mfuko wa Tasaf zinakwenda kwa watu wengine ambao hawahusiki kabisa.
Mhe. Kikwete amesema sio sawa fedha hizo zikatumika kinyume kwa kuwaingiza kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini watu wasiostahili.