Bila Visa
Kenya
Masai Mara, Pwani ya Diani
Bila Visa
Masai Mara, Pwani ya Diani
Bila Visa
Gorila, Ziwa Kivu
Bila Visa
Le Morne, Port Louis
Visa Uwasili
Burj Khalifa, Desert Safari
Visa Uwasili
Overwater Villas, Diving
Bila Visa
Safari, fukwe za pwani, na Nairobi yenye nguvu
Bila Visa
Nchi ya milima elfu, gorila, na mji safi
Chanzo cha Nile, mlima Rwenzori na wanyamapori
Ziwa Tanganyika na utamaduni wa kipekee
Pwani nzuri, chakula cha baharini na visiwa
Ziwa kubwa lenye maji safi na watu wakarimu
Maporomoko ya Victoria na hifadhi za wanyama
Maporomoko ya Victoria na Great Zimbabwe
Accra yenye nguvu, historia na pwani ya dhahabu
Dakar, muziki, na chakula kitamu cha Afrika Magharibi
Cape Town, safari na divai za kiwango cha juu
Bila Visa
Kisiwa cha paradiso, fukwe na milima ya kijani
Visa Uwasili
Mji wa kisasa, Burj Khalifa na ununuzi wa anasa
Visa Uwasili
Visiwa vya paradiso, maji ya samawati na resorts
Kuala Lumpur, vyakula vya mitaani na misitu ya mvua
Bali, hekalu za kale na chakula kitamu
Angkor Wat na utamaduni wa Khmer
Himalaya, Everest na hekalu histori
Doha ya kisasa, makumbusho na jangwa
Historia ya kale, usanifu wa ajabu na wageni
Utamaduni tajiri, sanaa na historia ya uhuru
Kisiwa cha asili, maporomoko na misitu ya mvua
Visiwa vya paradiso katika Bahari ya Pasifiki
Volcano, scuba diving na utamaduni wa asili
Tanzania ni kitovu cha utalii duniani. Gundua vivutio vya kipekee vilivyopo katika nchi yetu kuanzia mbuga za wanyama hadi fukwe safi.
Muda bora: 12:00 - 03:00 Asubuhi. Furahia asili, mapango ya popo, na hewa safi nje kidogo ya mji.
Kimbia na upepo wa bahari kuanzia Coco Beach hadi Daraja la Tanzanite. Muda bora: 11:30 Jioni.
Zunguka Posta na Upanga usiku. Jionee majengo ya kihistoria yakiwa yamewaka taa bila foleni.
Gundua ladha halisi za mtaani. Mishkaki, chips mayai na kahawa ya moto. Anza: saa 1:00 Usiku.
Kutoroka kelele za jiji. Safari ya boti dakika 20 tu kufurahia samaki wabichi na fukwe tulivu.
Una ndoto za kusafiri nje ya Tanzania? Hatua ya kwanza ni kupata pasipoti. Hapa ni mwongozo kamili wa jinsi ya kuomba pasipoti ya Tanzania kupitia Idara ya Uhamiaji.
Nenda www.immigration.go.tz β Huduma za Uhamiaji (eService) β Ombi Jipya
Jaza taarifa binafsi, wazazi, dhumuni la safari, na watu wa dharura. Hakikisha taarifa zako zinafanana na NIDA na cheti cha kuzaliwa.
Baada ya kuhakiki taarifa, lipa Sh20,000 kupitia namba za kumbukumbu. Kisha pakua na uchapashe fomu.
Wadhamini wawili watajaza na kutia sahihi. Peleka kwa Wakili au Mwanasheria kuthibitishwa na kugongwa mhuri.
Peleka fomu na viambata vyote (nakala na halisi). Una tiketi ya karibu? Iambatanishe ili ombi lifanyiwe kazi haraka.
Baada ya mahojiano, lipa Sh130,000. Utapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole.
Kumbuka: Malipo yote yanafanyika kupitia namba za kumbukumbu β si mkononi. Fuatilia maombi yako mwenyewe bila kutumia vishoka.
Kusafiri si burudani tu β ni uwekezaji katika maisha yako. Hizi ni sababu muhimu za kwa nini kila Mtanzania anapaswa kupanga safari angalau mara moja kwa mwaka.
Kusafiri kunakufungua macho kuona jinsi watu wengine wanavyoishi, kufikiria, na kutatua changamoto. Unarudi nyumbani na mtazamo mpya wa maisha.
Kujifunza utamaduni mpya na hata maneno machache ya lugha nyingine kunaimarisha uwezo wako wa kuwasiliana na watu duniani kote.
Safari hufungua milango ya biashara mpya. Utagundua bidhaa, huduma, na njia za mapato ambazo hazipo Tanzania lakini zinaweza kufanya kazi vizuri hapa.
Kutembelea nchi nyingine ni darasa kubwa zaidi ya chuo chochote. Unajifunza historia, teknolojia, na mbinu mpya za maisha kwa kuona na kushiriki.
Tafiti zinaonyesha watu wanaosafiri mara kwa mara wana msongo mdogo wa mawazo na furaha zaidi. Kubadili mazingira huburudisha ubongo.
Kunavigeti nchi mpya, kuzungumza na wageni, na kutatua changamoto za safari kunakujenga ujasiri na uwezo wa kukabiliana na hali yoyote.
Picha, hadithi, na uzoefu wa safari ni hazina ambazo huwezi kununua. Kila safari inakuwa sehemu ya hadithi ya maisha yako.
Wasanii, waandishi, na wajasiriamali wengi wanapata msukumo wao mkubwa kutokana na safari. Mazingira mapya huchochea ubunifu.
Kidokezo: Anza na nchi jirani kama Kenya, Uganda, au Rwanda β ziko karibu, bei nafuu, na huhitaji visa. Safari yako ya kwanza haipaswi kuwa ghali!
Kitambulisho cha NIDA ni hitaji muhimu kwa huduma nyingi za kiserikali na kijamii nchini Tanzania.
Pata barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa mtaa unapoishi.
Pakua fomu mtandaoni au chukua katika ofisi za NIDA za wilaya yako.
Fika katika ofisi za NIDA ukiwa na viambata (Cheti cha kuzaliwa, nk) kwa ajili ya picha na vidole.
Baada ya uhakiki, utapewa namba ya utambulisho (NIN) kupitia SMS au mtandaoni.
NCard ni mfumo wa malipo wa kielektroniki unaotumiwa kulipia huduma mbalimbali kama vile usafiri wa mwendokasi na viwanja vya michezo.
Unaweza kupata NCard katika vituo vikubwa vya basi (mwendokasi), maduka ya mawakala, au viwanja vya michezo.
Gharama ya kadi ni Sh5,000 tu. Unaweza kuweka salio (top-up) kupitia mawakala au benki za simu (M-Pesa, Tigo-Pesa, nk).