Akizungumzia kaulimbiu ya Nanenane ya mwaka huu isemayo “Tambua Soko, Ongeza Tija, Tekeleza Dira ya Taifa 2050,” Prof.Epaphra Manamba amesema dira hiyo inalenga kujenga nguvu kazi yenye ujuzi na maarifa inayoweza kuleta mapinduzi katika sekta mbalimbali za uchumi, hususan kilimo.
Kwa upande mwingine, amesema kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unategemea kwa kiwango kikubwa mageuzi ya sekta ya kilimo, ikiwemo mazao, mifugo, uvuvi na misitu, ambayo ndiyo msingi wa kukuza viwanda, biashara na uchumi wa nchi.
