Twiga Stars imeondolewa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ivory Coast katika mchezo wa mwisho wa Kundi B uliochezwa jijini Casablanca, Morocco.
Ndoto za timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2026) zimehitimishwa rasmi baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Ivory Coast.