Kikwete alibainisha kuwa Tanzania imeorodheshwa katika Kundi A la nchi zenye ukomavu wa juu wa matumizi ya teknolojia serikalini (Extensive GovTech Maturity), kwa mujibu wa tathmini ya Benki ya Dunia.
Tanzania imeendelea kung’ara kimataifa baada ya Benki ya Dunia (World Bank - WB) kuitaja kuwa miongoni mwa nchi zilizo na ukomavu wa juu wa matumizi ya TEHAMA katika sekta ya umma, hatua inayothibitisha mafanikio ya mageuzi ya kidijitali yanayoendelea kutekelezwa na Serikali.