Mhe. Balozi Omar pia alisisitiza kuwa utafiti ni nguzo muhimu ya maendeleo ya sekta za uzalishaji, hivyo uwekezaji katika taasisi za utafiti, ikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), ni muhimu ili kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya mifugo kupitia teknolojia na ubunifu wenye tija.
Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa uwekezaji huo unaofanywa na Serikali katika utafiti wa kilimo ni mwelekeo sahihi wa mageuzi katika sekta ya kilimo.
Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika utafiti wa kilimo na mifugo kwani maeneo hayo yana uwezo mkubwa wa kuleta mageuzi ya uzalishaji endapo yatapatiwa rasilimali za kutosha.