Mfanyabiashara na mtangazaji wa utalii, Khalid Hamed Al Barwani,, ameikabidhi Serikali gari la kihistoria aina ya Jeep Wrangler alilotumia katika safari kutoka Oman hadi Tanzania kama zawadi kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan, huku akiteuliwa kuwa Balozi wa Hiari wa Utalii Tanzania kutokana na mchango wake katika kuitangaza Tanzania kimataifa.
Mwanautalii na mtangazaji wa vivutio vya utalii kutoka Oman, Khalid Hamed Al Barwani, aliyesaidia kulitangaza kimataifa Shamba la Miti Sao Hill baada ya kuitembelea mwaka 2024, amekabidhiwa rasmi Ubalozi wa Hiari wa Utalii wa Tanzania katika hatua inayotarajiwa kuimarisha kampeni za kuitangaza nchi na kuongeza idadi ya watalii.