Tech & Science
The latest in technology and scientific discoveries
What's Happening
YAS YAONGEZA MINARA MIWILI YA 5G ARUSHA, YAAHIDI HUDUMA ZA VIWANGO
Wakazi wa jiji la Arusha wanatarajiwa kunufaika na huduma bora zaidi za mawasiliano na intaneti yenye kasi kufuatia uwekezaji mpya wa kampuni ya mawasiliano ya Yas kuongeza minara miwili ya teknolojia ya 5G jijini humo.Uwekezaji huo umeongeza idadi ya minara ya 5G ya Yas jijini Arusha kufikia 15, huku ikiwa na jumla ya minara (20) ya 4G. Uzinduzi huo ni muendelezo wa kuimarisha upatikanaji wa hudu
Wabuni mfumo wa kidijitali kubaini hewa hatarishi katika makazi
Katika hali ya kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa hali ya hewa jijini Dar es Salaam, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) wamebuni mfumo wa kisasa wa kiteknolojia unaolenga kufuatilia hali ya hewa na kutoa taarifa za uwepo wa gesi hatari na vichafuzi katika mazingira.
Sh405 bilioni kutekeleza vipaumbele sita Wizara ya Afya
Wizara ya Afya imeomba kuhidhinishiwa Sh405.89 bilioni kutekeleza vipaumbele sita ambayo vitajikita katika, kuimarisha utoaji huduma, ujenzi wa miundombinu ya afya, vifaa tiba, kuimarisha mifumo ya kidijitali na kuimarisha nguvu kazi ya wizara kwa kuajiri.
Sh405 billion allocated for six health sector priorities in Zanzibar
The Ministry of Health in Zanzibar has requested parliamentary approval of Sh405.89 billion to implement six priority areas aimed at improving healthcare delivery, infrastructure development, medical equipment, digital systems and workforce capacity.
Imani za kishirikina zinavyokwaza mapambano dhidi ya fistula
Imani za kishirikina na hofu ya unyanyapaa zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazoathiri juhudi za kutokomeza Ugonjwa wa Fistula nchini, huku wanawake wengi wakiamini hali hiyo husababishwa na uchawi badala ya matatizo ya uzazi.
Wanafunzi wa Veta waunda simu
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (Veta) Mkoa wa Pwani kimeingia hatua za mwisho za kubuni na kutengeneza simu ya mkononi kwa kutumia teknolojia ya ndani.
Nyumba yawaka moto, 24 wanusurika
Mbeya. Wanafunzi 24 wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) wamenusurika kifo baada ya nyumba wanayoitumia kama bweni kuungua moto, huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likitangaza operesheni maalumu. Tukio hilo linaelezwa kutokea jana Mei 18 majira ya saa nane mchana katika Mtaa wa Ikuti, Kata ya Iyunga jijini Mbeya. Wakati wa tukio hilo, wanafunzi hao hawakuwepo. Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema linatarajia kufanya operesheni maalumu kwa nyumba na mabweni yote yanayotumiwa na wanafunzi kuangalia ubora wake, ikiwamo mifumo ya umeme, na kutoa elimu kwa wamiliki na watumiaji. Akizungumza leo Jumanne Mei 19, 2026, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi hilo mkoani Mbeya, Malumbo Ngata, amethibitisha tukio hilo akisema hakuna madhara kwa binadamu zaidi ya mali zilizokuwamo kwenye nyumba hiyo katika vyumba sita vilivyowaka moto. Kamanda Ngata amefafanua kuwa nyumba hiyo iliyokuwa inatumika kama bweni ina jumla ya vyumba 24 huku sita kati ya hivyo, vikiteketea pamoja na samani zote zilizokuwa ndani. Hata hivyo, jeshi hilo likifanikiwa kuokoa vyumba 18 na mali zake. “Wakati wa tukio hakukuwamo mwanafunzi yeyote, hivyo hakuna vifo wala majeruhi kwa binadamu, zaidi ni vifaa kama magodoro kuungua katika vyumba sita ambavyo vimewaka moto. “Tunashukuru tukio lilikuwa mchana na Zimamoto tulifika kwa wakati na kuokoa vyumba 18 na mali zake. Chanzo bado hakijafahamika isipokuwa tunahisi moja ya vifaa vya hita kilichokuwa kimewashwa, ila tunaendelea na uchunguzi,” amesema. Amebainisha kuwa hilo ni tukio la pili kutokea jijini Mbeya. Awali, lilitokea maeneo ya Forest na kwamba wanatarajia kufanya operesheni maalumu kwa nyumba na mabweni yanayotumiwa na wanafunzi. Katika operesheni hiyo, amesema wataangalia mikataba baina ya vyuo na wamiliki wa nyumba, lengo likiwa kutoa elimu kwa watumiaji kuhusu usalama na kinga dhidi ya majanga ya moto. “Lakini tutataka kujiridhisha na ubora wa miundombinu ya nyumba zenyewe baada ya kupata orodha yake, kujua ubora wa mifumo ya umeme na kwa sasa Mbeya yetu ina baridi,” amesema. Kamanda Ngata amewataka wamiliki wa nyumba zinazotumiwa na wanafunzi kuhakikisha wanazingatia uimara wa miundombinu na watumiaji kuwa waangalifu wakati wa matumizi ya vifaa vya umeme. “Watoe taarifa pia inapotokea dharura ya moto kwa mamlaka, wahakikishe miundombinu ya umeme inakuwa na tahadhari za kupambana na majanga ya moto,” amesema. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Vaileth Msombwa, amesema wakiwa katika majukumu yao ya kila siku katika eneo hilo walishtushwa na moshi mkali uliokuwa ukitoka katika nyumba hiyo, hali iliyosababisha waliite Jeshi hilo. “Hatukujua, tulisikia tu kishindo cha moshi mzito ukifukuta kutoka kwenye nyumba hiyo na ukizingatia tunajua ni ya wanafunzi, tunashukuru Jeshi la Zimamoto lilifika haraka na huenda madhara yangekuwa makubwa,” amesema.
Mikoa hii ijipange kwa upepo mkali kuanzia kesho
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza matarajio ya uwepo wa upepo mkali wa kilomita 40 kwa saa katika mikoa mitano nchini.
Serikali kuharakisha sera ya matumizi ya akili unde, yasisitiza maadili
Serikali imejipanga kuharakisha kukamilika kwa Sera ya matumizi ya Akili Unde (AI) ili ianze kutumika rasmi na kutoa mwongozo wa matumizi ya teknolojia hiyo nchini.
TEKNOLOJIA YA MIZANI JANJA YATAJWA KUWA SULUHISHO KUONDOA UDANGANYIFU KATIKA VIPIMO
Kampuni ya Climb Up Limited imeeleza kuwa matumizi ya mizani janja ya kidigitali yanaweza kuwa suluhisho muhimu katika kuondoa changamoto za udanganyifu wa vipimo zinazowakabili wakulima, wafugaji na wafanyabiashara nchini.Akizungumza jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Emmanuel Ngallah, amesema teknoloji
Pillars
Chagua nguzo (pillar) ili kuona habari kwa undani kama ilivyo “leagues” kwenye Michezo.
Maendeleo makubwa Tanzania
Orodha fupi ya miradi/assembly na ubunifu unaoendelea kwenye sayansi na teknolojia.