Dk. Gwajima ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Serikali ili kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akisisitiza kuwa mafanikio ya maendeleo yanapaswa kuonekana kupitia mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, amezitaka asasi zisizo ya kiserikali (NGOs) kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na serikali ili kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
