Amesema Kurugenzi hiyo hufanya ukaguzi wa usalama na afya mahali pa kazi, hufuatilia utekelezaji wa mipango ya usimamizi wa mazingira, urejeshaji wa maeneo yaliyochimbwa pamoja na mipango ya ufungaji migodi kwa kuzingatia viwango vinavyolinda mazingira na kuhakikisha rasilimali za madini zinatumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Tume ya Madini inatumia Maonesho ya Nanenane kama jukwaa la kutoa elimu kwa wananchi, wachimbaji na wadau wa sekta kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga, mbinu salama za uchimbaji, utunzaji wa mazingira pamoja na uhifadhi na matumizi salama ya baruti.
