Amesema katika jukwaa hilo wamekubaliana makampuni mawili kushirikiana ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Africa50 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya usafirishaji wa umeme.
Makubaliano hayo yanahusu ushirikiano kati ya TANESCO na Africa50 katika miradi ya usafirishaji wa umeme (transmission), mradi wa Mini LNG kati ya TPDC, Taqa Arabia na Africa50 kwa ajili ya kuchakata gesi asilia.