Licha ya marufuku hiyo, vyombo vya habari nchini humo vimechapisha taarifa zikidai kuwa rais huyo anaumwa mahututi, huku mitandao ya kijamii ikisheheni utani unaomwelezea kama ‘Rais anayefanya kazi kwa njia ya mtandao’ au ‘Rais anayefanya kazi akiwa nje ya nchi’.
Wakati mjadala huo ukiendelea nchini humo, mamlaka za Cameroon zilipiga marufuku mijadala kuhusu afya ya Biya Oktoba 2024, wakati alipokuwa amepotea kwa muda katika mazingira yanayofanana na ya sasa.