Wakulima wanaweza kutumia huduma ya Kilimo Pesa kupata mikopo kwa ajili ya shughuli za kilimo, pamoja na Afya Mkulima, inayowawezesha kupata bima ya afya kwao na familia zao.
Mhe. Mohammed alipongeza matumizi ya teknolojia katika kurahisisha huduma za kifedha kwa wakulima, akisema mifumo ya kidijitali ina nafasi muhimu katika kuongeza usalama wa malipo na kuwawezesha wakulima kuendesha shughuli zao kwa ufanisi zaidi.