Waziri Mkuu amewahimiza vijana nchini kutumia fursa zilizopo katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuwekeza katika uzalishaji wa kisasa unaotumia teknolojia na ubunifu.
Mhe. Nchemba alimpongeza mfugaji huyo kwa uthubutu na maamuzi ya kuwekeza katika ufugaji wa kisasa, akisisitiza kuwa vijana wengi wanapaswa kuiga mfano huo kwa kutumia maarifa na teknolojia kujiajiri, kuongeza kipato na kuchangia maendeleo ya taifa kupitia sekta ya kilimo na mifugo.