Ninaomba kutoa tena msisitizo wangu katika kutambua mahitaji ya soko kwanza ili kuzalisha kulingana na mahitaji ili kuwa na uhakika wa soko la mazao yetu ya kilimo na ufugaji.
Akizungumzia Kaulimbiu ya Mwaka huu ya 'Tambua Soko, Ongeza Tija, Kutekeleza Dira 2050', Mhe. Mzava amesema utekelezaji wake unapaswa kuanzia kwenye Mbegu na namna wakulima na wafugaji wanavyohudumia mashamba na mifugo.