Alumni Initiative to Fund School Projects for Tosamaganga's 100th Anniversary
Habari mpya za elimu Tanzania · maelezo ya Alumni Initiative to Fund School Projects for Tosamagan… · imesasishwa 3 Aug 2026 · habari mpya · masasisho · maelezo
Muhtasari
- Tunazindua rasmi maandalizi ya Jubilee ya Miaka 100 ya Shule ya Sekondari Tosamaganga, taasisi iliyoanzishwa mwaka 1926 na ambayo kwa kipindi cha karne moja imeendelea kuwa nguzo ya elimu bora, maadili na uongozi nchini.
- Ratiba ya maadhimisho inaanza Oktoba 8 kwa matembezi ya Jubilee na shughuli za usafi wa mazingira, zikifuatiwa na mbio za Fun Run Oktoba 9 zitakazowakutanisha Alumni, wanafunzi na wananchi.
- Akizungumza kwa niaba ya wahitimu wa zamani, Edward Nzalalila, aliyesoma Tosamaganga kati ya mwaka 1968 na 1971, alisema Jubilee hiyo ni fursa ya kurejesha shukrani kwa taasisi iliyowajenga viongozi na wataalamu wengi.
- Alisema Alumni tayari wamechukua jukumu la kuhakikisha shule inapata basi jipya la wanafunzi lenye thamani ya takribani Sh Milioni 150, ambalo litakuwa sehemu ya urithi wa maadhimisho ya miaka 100.
- Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1926 chini ya Misheni ya Kanisa Katoliki kabla ya baadaye kuingia chini ya usimamizi wa serikali, Tosamaganga imeendelea kujijengea sifa ya kuwa miongoni mwa shule zilizozalisha viongozi.