Wakulima na wafugaji wanaotembelea kwenye Maonesho ya 32 ya Wakulima na Wafugaji na Sherehe za Wakulima Nanenane Kanda ya Kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi - Njiro mkoani Arusha, wamekiri kupata elimu ya kilimo na ufugaji bora.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Nurdini Babu amebainisha kuw aMonesho ya 32 ya Wakulima na Wafugaji na Sherehe za Wakulima Nanenane Kanda ya Kaskazini yamekuwa na tija kubwa kwa wakulima kutokana na uwepo wa teknolojia rahisi na zakisasa pamoja na mbegu bora za kilimo na mifugo.
Zaidi ya waoneshaji 500 wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wanatarajia kushiriki Maonesho ya 32 ya Kilimo na Mifugo na Sherehe za Wakulima Nanenane Kanda ya Kaskazini kwa kujikita kwenye kutambua soko, kuongeza tija na kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.