Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amesema maonesho ya 32 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na sherehe za Wakulima Nanenane Kanda ya Kaskazini, yamekuwa Maonesha bora zaidi ambayo ni maandalizi ya Maonesho ya mwaka ujao ambayo yatakuwa kipindi cha Mashindano ya Mpira wa Miguu mataifa ya Afrika -AFCON 2026 mkoani Arusha.
jumla ya Waoneshaji 466 wameshiriki maonesho hayo huku takribani watu 100,000 wakitembelea Maonesho kwa ajili ya kujifunza teknolojia na huduma mbalimbali zinazohusiana na Kilimo, Ugugaji na Uvuvi.