๐ Jinsi ya Kupata Pasipoti ya Kusafiria
Una ndoto za kusafiri nje ya Tanzania? Hatua ya kwanza ni kupata pasipoti. Hapa ni mwongozo kamili wa jinsi ya kuomba pasipoti ya Tanzania kupitia Idara ya Uhamiaji.
Viambata Vinavyohitajika
- โ Cheti cha Kuzaliwa (cha mwombaji)
- โ Cheti au Kiapo cha kuzaliwa mzazi wa mwombaji
- โ Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- โ Picha moja ya hivi karibuni (kivuli cha rangi ya buluu)
- โ Ushahidi wa safari au shughuli anayofanya mwombaji
- โ Barua ya utambulisho kutoka Serikali za Mtaa
Hatua kwa Hatua
Tembelea Tovuti ya Uhamiaji
Nenda www.immigration.go.tz โ Huduma za Uhamiaji (eService) โ Ombi Jipya
Jaza Fomu ya Maombi
Jaza taarifa binafsi, wazazi, dhumuni la safari, na watu wa dharura. Hakikisha taarifa zako zinafanana na NIDA na cheti cha kuzaliwa.
Lipa Sh20,000 (Fomu)
Baada ya kuhakiki taarifa, lipa Sh20,000 kupitia namba za kumbukumbu. Kisha pakua na uchapashe fomu.
Wadhamini & Wakili
Wadhamini wawili watajaza na kutia sahihi. Peleka kwa Wakili au Mwanasheria kuthibitishwa na kugongwa mhuri.
Wasilisha Ofisi ya Uhamiaji
Peleka fomu na viambata vyote (nakala na halisi). Una tiketi ya karibu? Iambatanishe ili ombi lifanyiwe kazi haraka.
Lipa Sh130,000 (Pasipoti)
Baada ya mahojiano, lipa Sh130,000. Utapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole.
Gharama
Muda wa Kutoka
Kumbuka: Malipo yote yanafanyika kupitia namba za kumbukumbu โ si mkononi. Fuatilia maombi yako mwenyewe bila kutumia vishoka.