Wavuvi wanapaswa kukata bima kwa ajili ya vyombo vyao na maisha yao
Habari mpya za kilimo Tanzania · maelezo ya Wavuvi wanapaswa kukata bima kwa ajili ya vyombo vyao n… · imesasishwa 10 Aug 2026 · habari za kilimo · wakulima · mazao
Muhtasari
- Amesema kwenye maonesho hayo Kijiji cha Bima kilipokea wageni zaidi ya 4,000 huku wengine wakiwafikia kupitia vyombo vya habari ambapo aliwasihi wananchi kufika katika ofisi mbalimbali za Bima kwaajili ya kupata elimu.
- Amesema wavuvi wa mitumbwi pia wanapaswa kukata bima kwa ajili ya vyombo vyao na maisha yao, akieleza kuwa injini ya boti ikipata hitilafu mvuvi anaweza kufidiwa.
- Aidha, mvuvi akipata ajali ziwani na kufariki, familia yake inaweza kupata fidia huku akibainisha kuwa wavuvi wengi bado hawakati bima za vyombo vyao wala bima binafsi.
- Tunawasihi sana wananchi wawe na utaratibu wa kulinda shughuli zao za kilimo,ufugaji na uvuvi kwa kukata bima ambazo zitawasaidia pindi wanapokuwa wamepata majanga”,Amesema Isango Kwaupande wake Meneja wa Kanda ya Ziwa.
- Naye Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Kanda ya Ziwa, Stella Marwa alisema,shirika hilo linatoa bima za ajali na maisha ikiwemo bima ya kilimo inayomkinga mkulima dhidi ya ukame, wadudu, mvua nyingi na majanga.