TBA imeendelea kujidhihirisha kama taasisi yenye uwezo wa kutoa huduma za ujenzi na usimamizi wa majengo zinazokidhi viwango, si kwa taasisi za serikali pekee bali pia kwa sekta binafsi.
Mweli ameyasema hayo Agosti 6, 2026, baada ya kutembelea banda la TBA katika Maonesho ya Kilimo Nanenane Kitaifa yanayoendelea jijini Dodoma, amesema Wizara ya Kilimo imefanya kazi nyingi kwa kushirikiana na TBA.