Wakili Mwambaja ametoa kauli hiyo alipotembelea banda la TARURA katika Maonesho ya 49 ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika uwanja wa Dkt. John Malecela mkoani Dodoma.
Wakili Boniventure Mwambaja, amesema anaiona Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuwa ni miongoni mwa taasisi bora za maendeleo ya miundombinu barani Afrika kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017.