Profesa Chibunda alisema SUA pia imeanzisha utafiti wa kutumia bundi kudhibiti panya waharibifu wa mazao mashambani.
Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ameeleza kuvutiwa na matumizi ya ndege aina ya bundi katika kudhibiti panya waharibifu wa mazao, akisema ubunifu huo wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sua) unaweza kuwa mkombozi kwa wakulima, kwa kupunguza uharibifu wa mazao bila kutumia kemikali.
