Hii ni mara ya tatu tangu Rais Chapo alipoingia madarakani mwaka 2025, ikiwa ni ishara ya dhamira ya viongozi wa Tanzania na Msumbiji ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kirafiki, undugu na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.
Ziara hiyo inalenga kuendeleza uhusiano wa kidugu na kihistoria, ujirani mwema na ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.