Kwa upande mwingine, wamejadili umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Bandari za Antwerpen nchini Ubelgiji na Dar es Salaam, pamoja na fursa za ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Ghent na taasisi za elimu nchini Tanzania katika kukuza matumizi na ufundishaji wa lugha ya Kiswahili.
Viongozi hao walisisitiza juu ya ushirikiano kati ya Bandari za Antwerpen na Dar es Salaam.