Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi kuwa kikosi chake kipo kwenye hali nzuri ya kimwili na kisaikolojia kuelekea pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Stars kwenye Uwanja wa Airtel, Singida.
Wekundu hao wa Msimbazi, wanaonolewa na Kocha Steve Barker, wanaingia kwenye mchezo huo wakisaka alama tatu muhimu ili kuendeleza wimbi la ushindi.