MKONGWE wa soka la Brazil, Ronaldinho, amejiunga na klabu ya Ravenna inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini Italia. Ronaldinho (46), alistaafu mwaka 2015 lakini jana Agosti 20, 2026, alitangaza kurudi mzigoni baada ya miaka 11 ya kuwa nje ya soka la ushindani.
Ronaldinho amefikia makubaliano na Ravenna FC, klabu ya Italia inayoshiriki Serie C, ambapo atahusishwa na klabu hiyo si tu kama mwekezaji, bali pia kama mchezaji.