Rais Samia amezitaka Wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) katika kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi katika ngazi mbalimbali katika kutatua migogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa njia ya mazungumzo na kuzingatia maslahi ya pande zote.