Mhandisi Mramba amesema hatua hiyo imefikiwa kutokana na juhudi mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali kuhakikisha Watanzania wanahamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, hususan gesi ya LPG, ili kulinda afya za wananchi na mazingira.