Nderiananga pia aliwahamasisha wananchi kutembelea maonesho hayo kwa wingi ili kupata uelewa mpana kuhusu majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake, sambamba na kujifunza fursa zinazopatikana katika sekta za kilimo na mifugo.
Ameipongeza WRRB kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na kutoa wito kwa wadau wa sekta ya kilimo kuendelea kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Maonesho ya Nane Nane ya mwaka 2026 isemayo, "Tambua Soko, Ongeza Tija, Tekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050," kwa kuimarisha mifumo ya masoko, kuongeza tija katika uzalishaji na kuhakikisha wakulima wananufaika na fursa zilizopo katika mnyororo wa thamani wa mazao.