Rombo ametoa wito huo leo Alhamisi Agosti 13, 2026 wakati akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Toba Alnason Nguvila kwenye ufunguzi wa kongamano la kuendeleza sekta ya kilimo, lililoandaliwa na Chuo cha Mipango, Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Rombo ameyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na Mkutano wa Mabunge duniani IPU, unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu pamoja na Michuano ya soka ya AFCON 2027 pamoja na shughuli za utalii zinazoendelea, akisema matukio hayo yataleta watu wengi Mkoani Arusha, suala ambalo litakuwa fursa kwa watu mbalimbali ikiwemo wazalishaji wa bidhaa za kilimo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amesema maonesho ya 32 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na sherehe za Wakulima Nanenane Kanda ya Kaskazini, yamekuwa Maonesha bora zaidi ambayo ni maandalizi ya Maonesho ya mwaka ujao ambayo yatakuwa kipindi cha Mashindano ya Mpira wa Miguu mataifa ya Afrika -AFCON 2026 mkoani Arusha.
Hata hivyo amewakumbusha wakulima na wafugaji kutumia fursa ya uwepo ya Mashindano ya Mpira wa Miguu Mataifa ya Afrika - AFCON mwaka 2027, ambapo Mkoa wa Arusha utakuwa wageni wengi watakaohitaji huduma za kijamii ikiwemo chakula, hivyo wametakiwa kujiandaa kwa msimu huo wa mashindano.